Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Sep 6, 2017

HOSPITAL YA WILAYA KIGOMA YAKOSA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

Baada ya kukosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Wilaya ya Kigoma Baptist kwa muda mrefu, uongozi wa hospitali hiyo umeamua kuanza mchakato wa ujenzi wa chumba hicho ili  kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Rufaa ya Maweni.

Akieleza namna ambavyo wamejipanga katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Daktari Kilawa Shindo amesema hadi kufikia mwakani ujenzi huo utakuwa umekamilika huku akiitaka serikali kutoa ushirikiano ili  kukamilisha ujenz huo.

Kwa upande wake mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma DR Paul Chaote amesema ni bahati mbaya sana hospitali ya wilaya kukosa chumba cha kuhifadhia maiti na kutokana na sera ya afya iliyopo ni lazima hospitali pamoja na vituo vya afya kuwa na sehemu hiyo maalumu.