Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Sep 7, 2017

UKUSANYAJI MAPATO KIGOMA MKUU WA MKOA AVUNJA UKIMYA


Mkuu wa mkoa wa Kigoma brigedia jeneral mstaafu Emanuel Maganga ameziagiza halmashauri za mkoa wa Kigoma, kuwa na mipango bora itakayo saidia kufikia leo la kukusanya mapato ya ndani nakuepuka usumbufu wa kutofikia malengo hayo.

Maganga ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kasulu kilichofanyika hivi karibuni, ambapo sambamba na kuipongeza halmashauri hiyo kwa namna wanavyofanya vizuri katika ukusanyaji mapato, ameshauri kuwa na mipango thabiti ili kuongeza asilimia katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Ameongeza kuwa kunahaja ya halmashauri hiyo kuboresha vyanzo vya ndani ili kukuza utalii wa ndani utakao saidia kuongeza mapato katika halmashauri.

Aidha katika hatua nyingine Manganga ameitaka halmashauri hiyo kuchukua hatua dhidi ya viongozi wasio zingatia kanuni za utumishi jambo litakalo saidia kuondoa changamoto zitokanazo na watumishi wasio waadilifu.