Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Oct 19, 2017

MTO MALAGARASI WAWATESA WANANCHI UVINZA

Wananchi wa kijiji cha sunuka na ilagala halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wameiomba serikali kutengeneza miundombinu ya daraja katika kivuko cha mto malagarasi ili kuondokana na kero pamoja na changamoto zinazowakabili.

Wakizungumza na blog hii wakazi hao wamesema licha ya kuwepo kwa kivuko katika mto lakini bado wanaendelea kuhangaika kutokana na kivuko hicho kuchukua muda mrefu kuwavusha na kusababisha kuchelewa katika majukumu yao huku wakiiomba serikali iwasaidie kuwajengea daraja ili waondokane na adha hiyo.

"Ukiachilia mbali kuchelewa kwenye shughuri zetu wakina mama wajawazito wamekuwa wakipata shida kutokana na kuchelewa kwa kivuko hicho hadi Wakati mwingine hujifungulia kwenye kivuko au kupoteza maisha kutokana na kuchelewa kufika kituo cha afya" wamebainisha wakazi hao.

Blog hii imefanikiwa kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko ambaye amejibu maombi ya wananchi wake kuwa serikali iko kwenye mpango wa ujenzi wa daraja hilo ambao utaanza hivi karibuni.

"Niwaombe wananchi kuwa wavumilivu mana serikali inatambua kero hiyo ndio mana imeweka mpango wa mkakati wa kujenga daraja na kumaliza kabisa zinazowakumba wananchi kwa sasa" amesema Bi Mlindoko.