Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Nov 3, 2017

POLISI WA FFU WATUPIWA LAWAMA NA MADEREVA BODABODA

Kufuatia kamatakamata ya bodaboda inayofanywa na asikari wa kutuliza Ghasia FFU badala ya askali wa usalama barabarani mkoani Kigoma, madereva wa usafiri huo wamelalamikia kitendo hicho nakulitaka Jeshi la polisi kuingilia kati ili kuondoa adha hiyo wanayoipata.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva hao wamesema wamekuwa hawaelewi ni kwa nini askari hao wa wa kutuliza ghasia wamekuwa wakiwakamata ili hali wanatambaua kuwa wanaouhusika ni askari wa  usalama barabarani.

"Kinachoshangaza ni pale unapopigwa pini na Askari wa FFU tena akiwa na siraha Wakati kazi yao ni kufanya doria na kukamata waharifu lakini wao wanakuja kutukamata hata Kama huna kosa atatafuta kosa lolote tu ilimladi akukamate na mengine kufuata" walisema madereva hao.

Akitolea ufafanuzi wa malalamiko hayo Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Mkoani Kigoma Oscar Mmole amesema askari yeyote anauwezo wa kukamata kosa lolote na kumfikisha mara moja mtuhumiwa kwenye kituo cha polisi.

Hata hivyo Mmole amesema kuwa sheria inaruhusu mwananchi yeyote atakayekamatwa na askari kuuliza na kufahamu jina la askari pia kuhoji amekukamata kwa kosa gani.