Wakazi wa kijiji cha Bitare kilichopo kata ya Bitare wilayani Kigoma mkoani Kigoma, wamelazimika kulala katika chanzo cha maji kilichopo kijijini humo ili kupata maji kutokana na kero ya maji inayowakabiri baada ya mradi wa maji mkongoro one kuharibika.
Blog hii imefika katika chanzo cha maji kinacho tegemewa na mamia ya wakazi wa kijijini hicho, ambao hata hivyo wameamua kugeuza maporomoko ya chanzo hicho kuwa sehem ya kulala ili kuwahi foleni ya maji kwani inawalazimu kufika katika chanzo hicho usiku.
"Yani jamani tunalala tango macho, vitanda vyote tumeshahamishia huku visimani mana ili uwahi foleni unatakiwa ufike mtoni saa tisa usiku, pia shida ya maji inasababisha watoto wetu kila Siku kuugua minyoo na kuharisha na serikali ipo ila inashindwa kutusaidia " walisema wanakijiji hao.
Akijibu malalamiko ya wananchi hao, Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma Bw, Bwami Matiasi ambaye pia ni diwani wa kata ya Bitare amekiri kuwepo kwa tatizo la maji katika KATA yake huku akibainisha kuwa chanzo cha kero hiyo ni baada ya kuharibika kwa mradi wa maji mkongoro one ambao ulikuwa ukihudumia vijiji tisa kikiwemo Bitale.
"Jitihada za ukarabati wa mradi wa maji mkongoro one zinaendelea na kama halimashauri tumeomba pesa kwa shirika la BTC na wamekubali kutupa zaidi ya billion moja ili tuweze kufanya marekebisho na kurudisha huduma ya maji kwa wananchi" amesema Bw. Bwami.
Nae Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya maji mkoani kigoma Muhandisi Azizi Mtabuzi amesema tatizo la maji si bitare pekee bali maeneo mengi hasa vijijini maji yamekuwa changamoto kubwa.
"Ili kutatua Tatizo hilo serikali inajitahidi kupata pesa za ndani ili kutatua kero ya maji katika vijiji vyenye shida ya huduma hiyo" amesema.
Contacts. 0765617630
Email : sennyemmanuel@gmail.com