Wananchi wa kijiji cha Kazuramimba kata ya kazuramimba halmashauri ya wilaya ya uvinza mkoani kigoma wamemvua madaraka mwenyekiti wa kijiji hicho kwa tuhuma za ubadirifu wa mali za kijiji.
Akizungumza na blog hii, Mkuu wa wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko amedhibitisha kuvuliwa madaraka kwa mwenyekiti huyo na wanakijiji wake hivi karibuni katika mkutano wa kijiji.
Aidha Bi, Mlindoko amesema hatua zitakazo chukuliwa ni wajumbe wa serikali ya kijiji kumchagua mjumbe mmoja ambaye atashika nafasi ya mwenyekiti kwa muda ili shughuri za serikali ya kijiji ziendelee pia amethibitisha kurudishwa kwa fedha zilizo chukuliwa kwenye akaunti ya kijiji hicho.
Blog hii imezungumza na Mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Saidi Kibuye ambaye kwa upande wake amekana kuhusika na tukio hilo la ubadhirifu wa fedha nakudai kuwa ni jama za baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji kutaka kumuondoa madarakani.
Hata hivyo Kibuye amekanusha kurudisha fedha ambazo hapo awali mkuu wa wilaya amesema zimerudishwa kwenye akaunti ya Kijiji.
Contacts : 0765617630
Email :sennyemmanuel@gmail.com