WAKATI
Watanzania wakisubilia kupiga kura ya kuwachagua viongozi watakao waongoza
katika uchaguzi Mkuu utakaofanyia mweze Octoba mwaka huu, Wanasiasa mbalimbali
mkoani Kigoma wamejitokea kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuviwakilisha vyama vyao katika nafasi ya
Ubunge.
Mkoa wa Kigoma wenye Wilaya sita
ambazo ni pamoja na Wilaya ya Kigoma, Kasulu, Kibondo, Uvinza, Kakonko
na Buhingwe, katika uchaguzi wa mwaka huu umegawanywa katika majimbo nane ya
uchaguzi ambayo ni Kigoma Mjini, Kigoma Kaskazini, Kigoma Kusini, Kasulu Mjini,
Kasulu Vijijini, Buyungu, Muhambwe (Kibondo) na Manyovu (Buhigwe).
Aidha tayari wanasiasa kupitia vyama hasimu hapa
nchini Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
walishachukua fomu na kurudisha ili kupata ridhaa ya vyama vyao katika
kinyanganyiro cha nafasi ya Ubunge.
Katika
Jimbo la Kigoma mjini, waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kupitia CHADEMA
ni pamoja na Mwanasheria Daniel Rumenyela, Kabwar Shaban, Ally Mleh na Francis
Mangu. Wakati CCM wakiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoani hapa, Dk. Waridi
Amani Kaboulou, Elisha Zilikana, Gabriel Sospeter na Zuberi Madie.
Wakati
vyama hivyo pinzani vikiandaa wagombe ambao watapambana katika uchaguzi ujao
katika Jimbo hilo, Zitto Kabwe ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma
Kaskazini kupita CHADEMA kabla ya kufukuzwa, alichukua fomu ya Ubunge ili kugombea katika Jimbo la
Kigoma mjini kupitia chama kipya cha ACT.
Katika
Jimbo la Kigoma Kaskazini, waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kupitia CHADEMA
ni pamoja na Mjumbe wa Kuchaguliwa
Kamati kuu Taifa wa Chama hicho, Dk Yared Fubusa, Kamsige Fabian, Munisi Faraja
na Akrani John.
Wakati
CCM wakiwa ni Peter Serukamba aliyekuwa akiliwakilisha Jimbo la Kigoma Mjini,
Halimeshi Kahena Manyonga, Juma Athumani Matete, Robison Fulgence Lembo,
Mahwago Kayandabila, Hamisi Betese, Omari Mussa Nkwarulo, Dk. Ernest Rugiga na
Robert Yohana.
Jimbo
la Kigoma Kusini, waliochukua fomu na kurudisha kupitia CHADEMA) ni mtu mmoja
tu ambaye ni Bonyimana Michael. Wakati CCM wakiwa ni Nashoni Bidyanguze, Waziri
Mourice, Thomas M. Sengai, Gulamhussein Kiffu Shabani, Salum I. Sasilo, Iddi
Ndabona, Dr. Norbert N. Shemetse, Hasna Mwilima, Dr. Ernest Nsumila, Ally Ayubu
Kalufya, Manju Salumu Msambya, January Kizito, Dismas Clemence Malele, Jumanne
M. Hussein na Majaliwa Zuberi.
Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe kulia akimtambulisha Mbunge wa Kasulu Mjini aliyemaliza muda wake Moses Machali ambaye amejiunga rasmi na ACT-Wazalendo |
Katika
Jimbo la Manyovu (Buhigwe), waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kupitia
CHADEMA ni pamoja na Baslius Budida, James Japhet, Dk. Henry Wilsom na Balakuba
Ndoloma huku waliochukua kupitia CCM ni Albert Obama, Abia Mnyabari, Phillipo
na Kavejuru Eliadoli.
Katika
Jimbo la Muhambwe (Kibondo), waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kupitia
CHADEMA ni mtu mmoja ambaye ni Nick
Kilunga, wakati CCM wakiwa ni Eng. Atashiste Ndikije, Moshi Nyakamwe, Emmanuel
Gwegenyeze, Dk Joseph Tutuba, Jarud Tumaini, Dk. Witonze Erick, Edger
Mkosamali, Regina Kayabu, Dk. Richard Kijarabs, Mapigano Nduhirubusa, Anderson
Njiginya.
Jimbo
la Buyungu, waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kupitia CHADEMA ni pamoja
na Kasuki Samson, Jiles Rungwana, Olafu Kaboboye, Gaston Garubinand, Rose
Ntirulasanye, Ashura Mashaka. CCM ni
Eng. Christopher Chiza, Carlos Gwamagobe, Ernest Basaya, Liberi Ndabita, Modest
Apolinary na Nsakila Kabende
Sambamba
na hayo, Moses Machali aliyekuwa Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR Mageuzi
baada ya kukihama chama hicho na kujiunga na ACT, alichukua fomu ili
kukiwakilisha chama hicho katika jimbo hilohilo huku akiungana na Mrisho
Mzingwa, Askofu David Mpango na Hamza
Mtunu.