Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 28, 2015

MAN UTD YAMNASA SERGIO ROMERO

Klabu ya Manchester Utd imekamilisha usajiri wa Kipa Sergio Romero, aliyekuwa akiichezea klabu ya Sampdoria, na  amejiunga na vijana wa Louis Van Gaal baada ya kukamilisha muda wa mkataba wake na Sampdoria.
Romero aliwahi kucheza chini ya Van gaal katika timu ya AZ Alkmaar ya Uholanzi iliyotwaa ubingwa wa kombe la ligi ya Uholanzi mnamo mwaka wa 2009.

Kipa huyo ametia saini mkataba wa miaka mitatu na anatarajiwa kuchukua nafasi ya kipa wa akiba, Victor Valdes ambaye ameambiwa yuko huru kuihama klabu hiyo na Van Gaal.

Romero alikuwa katika timu ya taifa ya Argentina iliyofika fainali ya Copa America mwaka huu na kombe la dunia nchini Brazil mwaka uliopita.

Kwa sasa kipa huyo ameungana na wana-devils katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo nchini Marekani.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji waliofunzwa na Van gaal ambao wameungana naye Old Trafford wengine wakiwa ni Memphis Depay, na Daley Blind.

Hatua ya kumsaini Romero inaonekana ni kama njia ya kupiga jeki idara ya ulinzi katika Manchester United huku Mhispania, David De gea akiendelea kusakwa na ReaL Madrid.