BAADA
ya Uchaguzi wa Kiti cha Udiwani kata ya Kagera katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji
kuahirishwa kutokana na picha ya mgombea wa ACT-Wazarendo kukosekana kwenye
urodha ya wagombea, uchaguzi huo umefanyika jana na kumalizika kwa amani huku
ACT ikiendelea kujiongezea viti vya udiwani.
Baada
ya uchaguzi na uhesabuji wa kura kumalizika, Mismamizi Mkuu wa uchaguzi katika
kata hiyo Stanslaus Ntatiye, ametangaza matokeo ambapo mgombea
Ismail Mahmud Hussein ACT alipata kura 959, Keberezo Gregory Fednand CCM 9 kura 18, Damas Rashid CHADEMA kura 497,
Mary Jeremiah – Jahazi Asilia kura 8.
Kwa
mujibu wa idadi hiyo ya kura, Msimamizi Ntatiye, amemtangaza Ismail Mahmud
Hussein wa ACT kuwa Diwani mpya wa kata ya Kagera huku akiungana na madiwani
wengine 18 waliochaguliwa Octoba 25.
Ushindi
huo wa ACT-Wazarendo umewafanya kuongeza viti vya udiwani na kuongoza katika
manispaa hii kwa kuwa na viti 13 wakati CCM ikiwa na viti vitano na CHADEMA
kiti kimoja tu.