UONGOZI
wa shule ya secondary Magaba iliyoko katika kijiji cha Nyakitonto Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umeadhimia kutoa elimu
bure kwa watoto wanaotoka katika familia maskini pamoja na wenye ulemavu wa
viungo.
Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne katika shule ya Secondary Magaba wakiwa kwenye mahafari ya yao na ya pili kwa shule hiyo. |
Hayo
yalibainishwa hapo jana na Mkurugenzi na
mmiliki wa shule hiyo Leonard Magaba wakati akizungumza na wazazi, walezi, wanafunzi wa
shule hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya wilaya ya Kasulu katika
mahafari ya pili yaliyofanyika shuleni hapo.
Magaba
alisema kuwa , kutokana na kutambua kuwa jamii ya kitanzania bado inakabiliwa
na umasikini wa kipato sambamba na baadhi ya watoto kushindwa kusoma kwasababu
ya ulemavu, shule hiyo itawagharimia
watoto hao ili nao wapate haki yao ya kuelimika.
Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne katika shule ya Secondary Magaba wakiwa kwenye mahafari ya yao na ya pili kwa shule hiyo. |
“Sikufanikiwa
kusoma hadi elimu ya juu japo nilikuwa napenda kusoma kutokana na wazazi wangu
kuwa na uwezo mdogo kifedha lakini hata hivyo ninamshukuru Mungu kuwa hivi
nilivyo, malengo ya kujenga shule ili
niwasaidie ndugu zangu yametimia na sasa nimekuwa na mchango kwa kuisaidia
jamii yangu’’ Alisema Bw. Magaba
Mkurugenzi na mmiliki wa shule ya secondary Magaba Leonard Magaba wa tatu kutoka kushoto akiwa na viongozi wa serikali katika mahafari ya kumali kidato cha nne katika shule yake. |
Alisema
kuwa, kuanzia mwakani 2016 shule yake imeweka utaratibu wa kuchukua mwanafunzi
mmoja kutoka kila shule ya msingi ndani ya kata hiyo ya Nyakitonto na
kumsomesha bure kwenye shule yake hadi kidato cha nne ila walengwa ni wanafunzi
waliofauru huku wakiwa ni yatima wasiokuwa na uwezo kifedha, walemavu ama
watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
“Mpaka
sasa natambua kwamba kuna watoto waliopo shule za misingi na wanafauru mitihani
yao ya kwenda sekondari lakini wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na
umasikini uliokithiri, sasa ili kuisaidia serikali kuhsu suala la elimu watoto
hao nitawapatia elimu ili nao wajitengenezee maisha ya baadae’’ alisema Magaba.
Magaba
aliongeza kuwa, kadri Mungu
atakavyomjalia ataongeza utaratibu huo na kuchukua wanafunzi katika ngazi ya
tarafa, Wilaya na hadi mkoa ili kuwasomesha pia amewataka wanajamii kushiriki
kwa kuwachangia watoto na jamaa zao kuwasomesha ili kupigana na adui ujinga.
Kwa
upande wao wazazi na wadau mbali katika sekta ya elimu walifurahishwa na kauli
hiyo na kuzitaka shule zingine binafsi kuiga mfano huo kwani utasaidia
kuwakomboa watoto walio katika mazingira hayo ambao wamekuwa wakishindwa kupata
elimu kutokana na ugumu wa maisha.
Obadia
Mbonye ambaye ni mmoja wa wazazi hao alisema kuwa maamuzi hayo ni ya kuigwa na
kwamba yatasaidia kuokoa watoto ambao wamekosa fursa ya kuendelea na elimu ya
sekondari kutokana na kuwa masikini wa kipato ama walemavu huku wakiwa na uwezo
wa kitaaluma.
Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne katika shule ya Secondary Magaba wakiwa kwenye mahafari ya yao na ya pili kwa shule hiyo. |
“Mtoto
ukimlea katika njia impasayo kamwe hataiacha hadi akiwa mzee na Tanzania
inahitaji vijana waliosoma na sio wanaoshinda vijiweni kwa kukosa ajira,
kitendo cha kuwasomesha watoto wasiojiweza ni cha kuigwa na jamii nzima kwa
lengo la kuinua elimu hapa nchini” alisema Ngoswe.