Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 12, 2016

KIKOSI BORA CHA FIFA 2015 BAADA YA UTANGAZWA JANA




Kikosi bora cha FIFA (FIFA/Fifpro World XI) mwaka 20015 kimewajumisha mlinda mlango wa Bayen Munich Manuel Neuer, Dan Alves, Marcelo, Thiago Silva, Sergio Ramos, Luca Modric, Andea Iniesta, Paul Pogba, Lion Messi, Christano Ronaldo na Neymar.

Klabu ya Real Madrid na FC Barcelona ndiyo timu zenye wachezaji wengi kwenye kikosi hicho zikiwa zimetoa wacheza wanne kwenye timu hiyo bora ya mwaka.


Golikipa wa Manuel Neuer wa Bayern Munich ndiye mchezaji pekee anayewakilisha ligi ya Ujerumani. EPL ndiyo ligi pekee kati ya ligi tano za juu za Ulaya kutotoa mwakilishi hata mmoja kwenye kikosi hicho.


Kocha wa Barcelona Luis Enrique ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka baada kukiongoza kikosi chake kutwaa mataji matano kati ya sita ndani ya mwaka 2015 lakini yaliyompa heshima kubwa ni mataji matatu (treble) Champions League, La Liga and the Copa del Rey.

Luis Enrique amemshinda kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ambaye alikuwa wapili wakati mshindi wa Copa America Jorge Sampaoli akimaliza nafasi ya tatu.

Mchezaji wa Atletico Goianiense Wendell Lira ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka (Puskas award)



Kiungo wa United States Carli Lloyd ambaye alifunga bao tatu kwenye fainali ya kombe la dunia ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanawake.

Kocha wa USA Jill Ellis amempiku kocha wa England Mark Sampson kwenye tuzo ya kocha bora wa soka la wanawake.

Hii ni Orodha ya washindi wa tuzo ya Ballon d’Or tangu mwaka 2003 mpaka 20014 ambapo mwaka 2015 imenyakuliwa na Messi.