Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 22, 2015

MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA WAAPISHWA TAYARI KUANZA KAZI

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma wameapishwa rasmi katika kikao cha kwanza cha madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ina madiwani 23 ambao wanwakilisha kata zao na wote waliapishwa na Jaji John Joshua (sio jina lake kamili).

Sambamba na kuapishwa madiwani hao walimchagua mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na makam wake ambapo Diwani Enock Jonas wa Kata ya  Nyarubanda ndie alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kupata kura zote 23.

Nafasi ya Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ni Diwani Gwamo John wa kata ya Bitale baada ya kuchaguliwa kwa kura 22 ambapo kura moja ya hapana ili wa ya Diwani wa kata ya Kalinzi Swage Dhahiri.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa.



Mbunge wa Kikogma Kaskazini Mh. Peter Serukamaba akiapa kuitumikia halmashauri hiyo kwa miaka mitano.
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Enock Jonas, akizungumza na madiwani baada ya kuchaguliwa katika kikao chao cha kwanza.
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Gwami John ambaye ni Diwani wa Kata ya Bitale akizungumza mara baada ya kuchaguliwa.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakiapa mbele ya Jaji John Joshua (Sio jina lake halali)





Mwisho.