Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 23, 2015

WATU SABA WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 10 KUJERUHIWA KATIKA AJARI YA GARI KUUNGUA MOTO KIGOMA

Watu saba wamefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa baada ya kutokea ajari ya gari aina ya Toyota Hiace lenye namba T.700 kupinduka na kuwaka moto katika Kijiji cha Mwakizega Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Mkoa ya Maweni, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Leonard Subi, amesema kuwa, jana majira ya jioni walipokea miili ya watu 6 waliofariki na majeruhi 11 baada ya kuungua katika ajari hiyo.
Majeruhi wa ajari ya gari kuwaka moto Mkoani Kigoma akipatiwa matibabu katika Hospitari ya Mkoa ya Maweni
 Amesema kuwa, wakati wakiendelea kutoa matibabu kwa majeruhi, mmoja wao  alifariki duni usiku wa kuamkia leo kutokana na kuungua vibaya hivyo idadi ya waliofariki kufikia saba ila  majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu.

“Miili ya marehemu imeifadhiwa katika chumba cha maiti na taratibu za kuitambua miili hiyo inaendelea ambapo miili mine imeshatambulika lakini mingine mitatu bado haijatambulika kutokana na kuu ngua vibaya”  amesema Dkt. Subi.
Majeruhi wa ajari ya gari kuwaka moto Mkoani Kigoma akipatiwa matibabu katika Hospitari ya Mkoa ya Maweni.
 Akielezea ajari hiyo  Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui, alisema kuwa tukio lilitokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo gari hilo lilikuwa  likitokea Kigoma mjini kuelekea Kijiji cha Subankara.

Amesema kuwa, chanzo cha ajari hiyo ni baada ya dreva kujaribu kuwakwepa watembea kwa mguu waliokuwa wakikatiza barabarani ambapo gari lilielekea upande mwingine ambapo liligonga ukingo wa barabara na kuangua kasha kuwaka moto.
Majeruhi wa ajari ya gari kuwaka moto Mkoani Kigoma, wakipatiwa matibabu katika Hospitari ya Mkoa ya Maweni.
“Walifariki katika ajari hiyo ni pamoja na Ashura Mussa (43), Kadogo Yusuph (20), Kabwe Idd (43), Mwamvua Juma na Peter Sungura miili miwili bado haijatambulika na waliojeruhiwa ni pamoja na Andrew Petro (59), Amos Thomas (20), Mutta Hamis (31), Shaban Fadhiri (54), Hasani Kasa (37), Essau Elias (20), Asha Kassim (38) na Riziki Jaah (9)" amesema Kamanda Mtui.

Hata hivyo Kamanda Mtui amesema kuwa, baada ya tukio hilo dreva wa gari lile Mohamed Mfaume (35) alikimbia kusikojulikana na Jeshi la Polisi wanaendela kumtafta ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Majeruhi wa ajari ya gari kuwaka moto Mkoani Kigoma akipatiwa matibabu katika Hospitari ya Mkoa ya Maweni.