Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 2, 2015

WATOTO WAWILI WAFARIKI BAADA YA KUUNGUA MOTO



WATOTO wawili wanaojulikana kwa majina ya Maiko Rajabu (6) na Abdallah Rajabu (4) wamefariki dunia baada ya kutokea kwa ajari ya moto maeneo ya Kichwele katika Kata ya Gungu Manispaa ya Kigoma –Ujiji mkoani Kigoma.
  
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea Novemba 27 majira ya saa 7:00 asubuhi baada ya nyumba ya Rajabu Maiko (37) kuungua moto na kusababisha vifo vya watoto wake Maiko Rajabu (6) na Abdallah Rajabu (4).

“Watoto wale waliachwa na mama yao wakiwa wamelala chumbani ambapo aliwaaga kuwa anaenda kwa Mjumbe wa Mtaa, Chanzo cha moto ule hakijajulikana na uchunguzi wa tukio unaendelea ili kubaini chanzo chake” alisema Kamanda Mtui

Kamanda Mtui alitoa wito kwa wazazi kuwaaangalia watoto wao kwa ukaribu ili kuepusha kutokea kwa matukio kama hayo.