Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 7, 2015

MWANAMKE AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA ROLI LA MIZIGO


Mwanamke mmoja mkazi wa Kagunga katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma anaejulikana kwa jina la Annastazia Ndihagati (51) amefariki dunia papo hapo baada ya kuangukiwa na gari kubwa la mizigo.

Tukio hilo limetokea Decemba 4 majira ya saa kumi alasiri  katika kata ya kumsenga mtaa wa Kagunga baada ya gari lamizigo (semitrela) kukwama kwenye matope yaliyosababishwa na mvua iliyokuwa ikinyesha na wakati dreva akijaribu kulikwamua gari lile likaanguka na kumwangua mwanamke yule  na kufariki papo hapo.
Akizungumza na blog hii kuhusu tukio hilo kaka wa marehem Khatibu Kasunzu alisema  kuwa gari lilimuangukia dada yake mwenye tatizo la mguu kutokana na kuwa na mzigo mkubwa ndani yake pamoja na uzembe wa dreva. 
Jeshi la polisi wilayani Kasulu lilifika katika eneo hilo na kusimamia ulinzi wa mzigo wote uliokuwa umepakiwa kwenye gari hilo ambao ilibidi mzigo uhamishwe kwenye magari mengine mawili na kufanikiwa kuliinua gari hilo majira ya saa sita usiku na kufanikiwa kuutoa mwili wa Bi annastazia ukiwa umeharibika vibaya.