WATU
wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa baada ya kushambuliana kwa risasi
na askari polisi waliokuwa kwenye dolia katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu
wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Akizungumza
na Waandishi wa habari hii leo, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, SACP Fednandi
Mtui alisema kuwa, tukio hilo lilitokea November 27 majira ya saa tisa alasiri
ambapo watu hao hawajafahamika hadi sasa huku miili yao ikiwa imehifadhiwa
kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospital ya wilaya ya Kasulu mkoani
hapa.
|
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akionyesha siraha aina ya SMG waliyokuwa nayo majambazi waliouwawa. |
Alisema
kuwa, awali watu hao walipola vitu mbalimbali na kukimbia navyo, baada ya raia
wema kutoa taarifa, polisi walifika na kufanya
msako hatimaye kuwakurupusha
majambazi hao waliokuwa wamejificha kwenye vichaka.
“Baada
ya kuwakurupusha walianza kurushiana risasi ambapo Polisi waliwajeruhi
na baada ya kuwakamata waliwapekuwa na kufanikiwa kuwakuta na siraha moja aina
ya SMG iliyokatwa mtutu na kitako, pia
walikuwa na magazine tatu huku mbili zilikuwa na risasi 60 na risasi zingine 33
zikiwa kwenye mfuko wa naironi” alisema Kamanda Mtui.
|
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akionyesha magazine ambazo ndani zina jumla ya risasi 59. |
Aidha
Kamanda Mtui alisema kuwa, vitu vilivyoibwa na watu wale kutoka kwa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu ni pamoja na simu mbili,
Vocha 45 za mitandao miwili tofauti pamoja na nguo mbalimbali.
Aliongeza
kuwa, kutokana na majeraha waliyokuwa nayo majambazi wale ilibidi wapelekwe
hospitali kwaajiri ya matibabu lakini kabla ya kufikishwa walifariki hivyo miili hiyo kuhifadhiwa kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti.
Hata
hivyo Kamanda Mtui aliwaomba wananchi kuendelea
kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kutoa taarifa pale wanapoona watu
wanaowatilia mashaka ili kudhibiti matukio kabla ya kutokea.
|
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akionyesha Vocha zilizoibwa kwa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu. |
|
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akionyesha Vocha zilizoibwa kwa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu. |
|
Risasi zilizokutwa ndani ya mfuko. |