Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 8, 2016

JKT YAITAKA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KUTOA TAARIFA SAHIHI KWA VIJANA



Makamanda wa gwaride wakiwaongoza washiriki wa mafunzo ya kujitolea katika kambi ya JKT Bulombora kutoa heshima kwa mwendo wa kasi kwa Mkuu wa mkoa Kigoma (Hayupo Pichani) wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo yanayojulikana kama Operesheni Kikwete.

Mkuu wa Mkoa Kigoma Issa Machibya (Mwenye suti) akikagua gwaride la vijana wa kujitolea Operesheni Kikwete  katika kambi ya Jeshi la kujenga Taifa Bulombora wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wakati wa sherehe ya kumaliza mafunzo kwa vijana 528 wa kujitolea.
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limezitaka kamati ya ulinzi na usalama ya mikoa na wilaya kutoa taarifa sahihi kwa vijana wanaotaka kujiunga na mafunzo katika kambi za jeshi hilo kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya kuwaandaa kuingia kwenye soko la ajira na sio sehemu ya ajira moja kwa moja kama wanavyofikilia wao. 


Akizungumza katika sherehe za kufunga mafunzo kwa vijana 528 yanayojulikana kama Operesheni Kikwete katika kambi ya JKT Bulombola Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Mkuu wa kambi ya kambi hiyo, Luteni Kanali  Mohamed Mketto, alisema kuwa, baada ya mafunzo hayo vijana wanaweza kupata ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama nchini pindi vyombo hivyo vitakapokuwa na mahitaji ya kuajii watumishi wapya.
Mketto alisema kuwa, vijana wengi wanapoanza mafunzo hudhani tayari wameajiriwa na jeshi na kwamba pindi mafunzo yanapomalizika vijana wengi hukata tamaa na kudhani ndiyo mwisho wakati wanayo fursa kubwa na nafasi kubwa ya kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi au kuanzisha miradi ya kuwaingizia kipato kutokana na juzi mbalimbali wanazozipata kambini humo.
kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kigoma Issa Machibya aliwataka vijana hao kutumia mafunzo kuwajenga katika uzalendo lakini pia kujihusisha katika shughuli za uzalishaji mali ambazo zinakuwa na manufaa kwa kwao na Taifa kwa ujumla.

"Ni jambo la aibu na fedheha kwa vijana wanaomaliza mafunzo na kujiingizia katika vitendo vya ujambazi, matumizi ya madawa ya kulevya na uasherati kwani serikali inayo mipango mingi kwa vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT nchini hivyo ni vyema kuwa wavumilivu na kutokukata tamaa mapema" alisema Machibya.
Awali katika risala ya washiriki wa mafunzo hayo, iliyosomwa na Gloria Kishai  waliitaka serikali kupitia katika jeshi hilo kuimarisha huduma za afya kwenye kambi ya Bulombora kutokana na changamoto zilizojitokeza mwishoni mwa mwaka jana ilipotokea ajali ya gari la kikosi hicho na kuua vijana saba na kujeruhi wengine 20.

"Tutatumia mafunzo tuliyopata kwa kufanyia kazi kwa vitendo ili kuendana na kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  John Magufuli ya Hapa Kazi Tu" alisema Kishai.