Vijana
wameomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wametakiwa kutumia mafunzo waliyopewa kwa
kushirikiana na jamii kwa kuwafichua waharifu na wahamiaji haramu na kuongoza
juhudi za kuimalisha usalama katika maeneo ya nchi kwa kushirikiana na jeshi la
polisi nchini chini ya farisafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.
Akizungumza
katika sherehe za kufunga mafunzo kwa vijana 528 yanayojulikana kama Operesheni
Kikwete katika kambi ya JKT Bulombola Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya, aliwataka vijana hao kujari
masrahi ya Taifa badara ya kujiingiza katika makundi ya uharifu ambayo huleta
hasara kwa taifa.
Alisema, vijana ndio uti wa mgongo wa Taifa hivyo wanawaangaliwa kwa jicho tatu hasa
katika kudumisha amani ya nchi.
Aidha
Machibya, aliwataka vijana hao kuwa mfano bora miongoni mwa vijana
wanaowazunguka katika maeneo yao hasa kwa kujiletea mafanikio kupitia mafunzo
waliyoyapata.