Klabu ya Manchester Unitrd imejikuta ikipoteza mchezo wake wa ligi baada ya kuambulia kipigo cha bao moja kutoka kwa Southampton katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Old Traford.
Bao pekee la Southampton lilifungwa na mchezaji mpya wa timu hiyo Charlie Austin ikiwa ni dakika saba baada ya kuingia akitokea benchi..
Kwa upande wa Liverpool wao walipata ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Norwich City na kuifanya timu hiyo kupanda hadi nafasi ya saba ya msimamo wa ligi.
Robert Firmino aliiweka kifua mbele Liverpool baada ya kufunga bao dakika ya 18 ya mchezo lakini Dieumerci Mbokani alisawazisha kwa upande wa Norwich kabla ya bao La Steve Naismith kuiweka mbele Norwich kwa mabao 2-1.
Wes Hoolan alifunga bao la tatu kwa penalti hivyo Norwich kuwa mbele kwa mabao 3-1 lakini baadae Jordan Henderson alifunga bao la pili kwa Liverpool na Frimino akaongeza bao la tatu na mchezo kuwa 3-3.
James Milner alifunga tena kwa upande wa Liverpool lakini baada ya muda Sabastian Basson akisawazisha na mabao yakawa 4-4 ila zikiwa zimesalia dakika 2 mpira kuisha Adam Lallana akafunga bao la Ushindi hivyo Liverpool kuondoka na ushindi wa mabao 5-4.
Matokeo mengine ni kama ifuatavyo.
Crystal Palace 1 - 3 Tottenham
Leicester 3 - 0 Stoke
Man Utd 0 - 1 Southampton
Sunderland 1 - 1 Bournemouth
Watford 2 - 1 Newcastle
West Brom 0 - 0 Aston Villa
West Ham 2 - 2 Man City