Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 23, 2016

CHELSEA NA LIVERPOOL NDANI YA BIFU ZITO

Klabu za Chelsea na Liverpool zimeingia kwenye vita kubwa ya kuwania saini ya mchezaji wa Shakta Donetsk, Mbrazil Alex Teixeira ambapo klabu yake inadai mchezaji huyo anathamani ya Paun mil. 39.

Klabu ya Liverpool ilikuwa inakaribia kumsajiri lakini kutokana na dau ililoweka la paun mil 24 kukataliwa na bado Liverpool wameshindwa kuongeza dau linalotakiwa na Shakta huenda wasiweze kumsajiri mchezaji huyo.

Wakati Liverpool wakisuasua kumsajiri Teixeira, Klabu ya Chelsea nayo imeingia katika mbio hizo la kumsajiri mchezaji huyo na kama chelsea watatoa pesa inayotakiwa na Shakta basi watakuwa wameipiku Liverpool kwa kumsajiri Teixeira.