Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Gerrard Guninita. aliyesimama. |
Akizungumza katika kikao cha madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Vijijini mkoani hapa. Mkuu wa Wilaya hiyo Gerrard Guninita alisema kuwa, walimu hao walikiuka agizo la Rais kwa kuwatoza wanafunzi pesa za ada na michango mingine.
Kwa kuthibitisha suala hilo Guninita alisema
kuwa, baada ya shule kufunguliwa alipita katika baadhi ya shule na kugundua
kuna baadhi ya walimu wanachukua pesa za kuwaandikisha wanafunzi sambamba
na michango mingine ikiwemo Compyuta.
“Sasa
kwakuwa walimu hao wanafanya hivyo huku wakiwa wanajua ni makosa, ninawapa wiki
moja wawe wamerudisha pesa hizo kwa wazazi wote na endapo wasipofanya hivyo
ndani ya wiki moja hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao” alisema Guninita.
Aidha Guninita aliwataka madiwani katika wilaya hiyo kuhakikisha
wanawaelimisha wazazi kuwapeleka watoto wao shule kutokana na vikwazo
vilivyotolewa ikiwemo ada na michango mingine.
"Kwa mzazi atakae shindwa kumpeleka mtoto shule kwa sababu zake binafsi
hatuta mvumilia tutamchukulia hatua hivyo ninaomba wazazi wote muhamasike kuwapeleka
shule watoto wenu" aliongeza Guninita.