Afisa Masoko wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kigoma, Evance Ndyamukama. |
Mfuko wa hifadhi ya Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Kigoma
umeanzisha huduma ya upimaji wa afya za kwa wakazi wa kigoma lengo ikiwa ni
kuwarahisishia huduma ya vipimo wakazi hao pamoja na kutoa hamasa kwa
wananchi kujiunga na mfuko huo.
Akizungumzia zoezi hilo meneja wa mfuko wa huo Mkoa wa Kigoma
Elias Odhiambo alisema, zoezi hilo lilianza jana mkoani hapo ambapo lengo kuu
ni kurahisha upimaji afya kwa wakazi hao sambamba na kutoa elimu kwa wakazi hao
kujiunga na mfuko wa Bima ya afya.
“tunatoa huduma ya vipimo bure ambapo tumewatangazia wananchi
iliwaweze kufika viwanja vya community centre mwanga mjini Kigoma lengo letu ni
wakazi wote kupata huduma hyo lakini pia tunawahamisha kujiunga na mfuko wa
bima ya afya ili kuona umuhimu wa malipo kabla” alisema Odhiambo.
Aidha alisema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia
jumatatu hadi ijumaa ambapo alisema vipimo vinavyotolewa ni urefu na uzito,
sukari, presha macho pamoja na huduma ya vipimo vya virusi vya ukimwi HIV ambayo
inetolewa kwa kushirikana na kitengo cha CTC cha hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Kigoma Maweni.