Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Feb 17, 2016

MAN UTD NA LIVERPOOL VITANI EUROPA

Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI itachezwa Wiki hii kwa Mechi 16 na England ina Timu 3 ambazo ni Manchester United, Liverpool na Tottenham.

Raundi hii imejumuisha Timu 24 zilizofuzu kutoka Makundi ya Mashindano haya na Timu 8 zilizomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ikiwemo Man United.

Timu hizi 3 za England zote zitaanza kucheza Mechi zao Ugenini hapo Alhamisi Februari 18 kwa Man United kucheza huko Denmark na FC Midtjylland, Tottenham, ambao walishiriki Mashindano haya kutoka hatua ya Makundi, wamepangiwa Klabu ya Serie A Fiorentina wakati Liverpool, ambao pia walikuwemo Makundi ya EUROPA LIGI, watacheza na Klabu ya Germany Augsburg.

Valencia ya Spain, ambayo ipo chini ya Mchezaji wa zamani wa Man United Gary Neville, watacheza na Rapid Vienna ya Austria wakati mtanange mkali wa Raundi hii ni ule wa Borussia Dortmund na FC Porto.

Ratiba ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32,

Jumanne Februari 16 
Fenerbahce vs Lokomotiv Moscow,

Alhamisi Februari 18
Sevilla v Molde,
Villarreal v Napoli,
Borussia Dortmund v Porto,
Anderlecht v Olympiacos,
Fiorentina v Tottenham,
St Etienne v Basle,
Midtjylland v Manchester United,
Valencia v Rapid Vienna,
Augsburg v Liverpool,
Sparta Prague v Krasnodar,
Galatasaray v Lazio,
Sion v Braga,
Shakhtar Donetsk v Schalke,
Marseille v Athletic Bilbao,
Sporting Lisbon v Bayer Leverkusen.