Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Feb 4, 2016

MARTINEZ AWEKA REKODI CHINA

Klabu ya soka ya Guangzhou Evergrande ya nchini China, imefanikiwa kufanya usajiri ambao unavunja rekod ya usajiri katika nchi hiyo baada ya kilabu hiyo kumsajiri mshambuliaji wa Atletico Madrid Jackson Martinez.
Klabu hiyo imelipa karibu dolla million 45 kumsajiri za mshambuliaji huyo raia wa Colombia, Martinez ambae sasa ameihama timu ya uhispania Atletico Madrid ametia sahihi kandarasi ya miaka minne.

Aliwahi kuifungia Atletico mabao 22 baada ya kuhamia Uhispania kutoka Porto.
Yeye ndiye mchezaji wa kiwango chake kuhamia Uchina baada ya kiungo cha kati wa Chelsea Ramires kuhamia Jiangsu Suning.

Si hao tu pia kuna Gervinho na Fredy Guarin waliohamia hukohuko China.
Kwa kutumia kitita kikubwa namna hiyo sasa ligi kuu ya Uchina inaikurubia ligi ya Uingereza kwa kima cha fedha zinazotumuka katika kuendesha soka nchini humo.

Ununuzi na usajili huo wa wachezaji umeshika kasi katika vilabu vya Uchina baada ya matamshi ya hivi karibuni ya rais Xi Jinping, ambae mwenyewe ni shabiki sugu, akisema kuandaa, kufuzu na kushinda kombe la dunia sasa ni miongoni mwa kipaumbele cha taifa hilo kubwa zaidi duniani.

Kocha wa Martinez katika klabu yake hiyo mpya ni kocha wa zamani wa Chelsea na Brazil ,Luiz Felipe Scolari.

Akiwa huko atajiunga na kiungo wa kati wa zamani wa Tottenham Paulinho na Robinho .
Kwa mujibu wa takwimu za gharama ya uhamisho ligi hiyo ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Uingereza.