Nafaka za mahindi ni moja ya nafaka zilizozuiliwa kuuzwa nje ya nchi. |
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga (Kushoto) akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia). |
Serikali
ya mkoa wa Kigoma imewataka wananchi kutambua kuwa bidhaa zilizozuiliwa kuuzwa
nje ya nchi ni Nafaka za Mahindi, Unga, Mchele, Mihogo na Mpunga na si kama
ilivyonukuliwa kwa bidhaa zingine ambazo hazijatajwa.
Ufafanuzi huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga alipozungumza na
waandishi wa habari hivi karibuni baada ya kuenea kwa uvumi kuwa
serikali imezuia uuzwaji wa bidhaa zote za chakula kwenda nje ya nchi kama Congo, Burundi na Rwanda.
Bwana Anga amesema kuwa bidhaa kama Viazi, Matunda ya aina zote pamoja na mboga mboga hizo zote zinaruhusiwa kuuzwa nje ya nchi hivyo taarifa zilizoenea kuhusu kuzuliliwa kwa bidhaa hizo sio kweli hivyo wananchi waendee kuuza bidhaa zao.
"Bidhaa hizo ziendelee kuuzwa bila woga ila kwa nafaka kama zilivyotajwa hizo ndio zimezuiliwa ili kufanya tathimini ya kiasi cha nafaka kilichopo" alisema.
Aidha
Anga amesema, kiliundwa kikosi kazi kwaajiri ya zoezi hilo ambalo
limeshakamilika hivyo muda si mrefu taarifa itatolewa ili kuendelea na uuzaji
kama kawaida .
Hata
hivyo Anga amesema wametoa maelekezo kwa wakuu wa Wilaya wote mkoani Kigoma kusitisha Zuio la Bidhaa tofauti na
zilizozuiliwa na Wizara ya Kilimo na Uvuvi na Mifugo.