Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Feb 1, 2016

WACHEZAJI WA AFRIKA WAKIMBILIA CHINA

Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina akitokea klabu ya Trabzonspor ya Uturuki.

Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 29 sasa atajiunga na nyota wa Ivory Coast Gervinho katika klabu hiyo ya Uchina, Gervinho alijiunga na Hebei China Fortune akitokea AS Roma Jumatano.

"Twamsubiri sana beki kamili Mbia afike hapa na kuonyesha ustadi wake,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter.

Mbia aliandika pia kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Najivunia kujiunga na Hebei China Fortune, niko tayari. Twende kazi."