Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Feb 2, 2016

GUADIOLA KOCHA MPYA MAN CITY

Kocha wa Bayer Munich Pep Guardiola amekubali kuchukua jukumu la kuifundisha Manchester City ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja mpya wa wa timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika.

Guardiola, atachukua majukumu hayo kuanzia Julai, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imetangaza.
Manuel Pellegrini ataondoka klabu hiyo Juni 30 baada ya kumalizika kwa msimu wa sasa.

"Kutokana na heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kufanya wazi uamuzi wake ili kuondoa nafasi ya uvumi,” City wamesema kupitia taarifa kwenye tovuti yao.

"Manuel, ambaye anaunga mkono kikamilifu uamuzi wa kufanya tangazo hili, anaangazia kutimiza malengo yake ya msimu huu na anadumisha kujitolea na heshima ambayo amekuwa nayo machoni ma wote wanaohusika katika uongozi wa klabu.”