VIONGOZI na wanachama 25 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa
wa Kigoma wamefukuzwa uanachama wa chama hicho kutokana na usaliti
uliofanyika ndani ya chama wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika oktaba
25, 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CCM
Mkoa Katibu wa CCM chama hicho mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema,
uamuzi huo umetolewa katika kikao cha halmashauri kuu cha Mkoa
kilichofanyika march 2016 kilicholenga kufanya tathimini ya uchaguzi
huo.
Naomi alisema kuwa baaada ya uchaguzi mkuu kufanyika chama
kilianza kufanya tathimini lengo ikiwa ni kubaini mafanikio pamoja na
changamoto zilizojitokeza katika chama hicho ili kujua nini kifanyike
kuepuka changamoto zilizojitokeza kipindi hcha uchaguzi huo.
Alieleza kuwa sababu mbali mbali zilizochangia wanachama
hao kuvuliwa uanachama ni kuhama chama kutokana na sababu ya kutoteuliwa
kuwa wagombea wa nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi huo na viongozi
waliosaliti chama kwa kutumia nguvu ya ushawishi wa kukiangusha chama
hicho pamoja na kugombe kupitia vyama pinzani baada ya kukosa nafasi
CCM.
''tulifanya tathimini na kugundua kuwa baadhi ya wanachama
ambao walikuwa siyo waaminifu kipindi cha uchaguzi mkuu walikuwa
wakikisaliti chama, hata viongozi waliogombea ubunge na kushindwa
kwenye kura za maoni tumewavua uanachama ili watupishe sisi tuendelee
kutekeleza ilani ya chama''alisema Kapambala.
Aidha wanachama waliofukuzwa ni Venance Mpologomi, Paul
bahinda, Damasi Shetei,Gidioni Bunyanga, Edger Mkosamali, Pili Waziri,
Pendo Jumanne, Robinson Lembo, Juma matete, Idd Lugundanya, Juma Kifuku,
Edga Bisoma, Staphord Kumuhanda, Jenoveva Bisana, Salehe Anatori,
Abdallah Chugu, Atanas Andrea, Bigilimana Vyanda, Jonas Kafyiri, Isack
Braytony, Christopher Chiza, Fanuel Kasogota, Laulent Bikulamuchi,
Ibramu Shikuzilya na Paul Chabandi.
Akizungumzia zoezi hilo Katibu wa jumui ya ya wazazi Mkoa
wa Kigoma Staney Mkandawile alisema, kwa sasa hivi kazi iliyopo ni
kutekeleza ilani ya chama na kuumunga mkono Rais John Magufuli kauli
mbiu ya hapa kazi tu ili kuweza kutekeleza majukumu ya Chama.
Mkandawile alisema kuwa Chama hakitamuonea aibu mwanachama
yeyote na kwamba bora chama kibaki na wanachama wachache ndani ya chama
ambao wapo tayari kufanya kazi za chama na kukipenda kwa dhati lengo
ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama hicho.