Mchezaji wa klabu ya Trabzonspor,
Salih Dursun, alitolewa nje kwa kumuonyesha mwamuzi kadi nyekundu wakati
wa mchezo waliofungwa mabao 2-1 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Uturuki.
Trabzonspor walikuwa tayari wamesalia wachezaji tisa uwanjani kabla ya kutokea kwa kisa hicho.
Wachezaji wa Trabzospor walimzingira mwamuzi kupinga kadi hiyo.
Ni wakati huo ambapo Dursun alimnyang’anya refa kadi nyekundu aliyokuwa nayo na kumuonyesha kadi hiyo hatua ambayo ilipelekea na yeye kufukuzwa uwanjani.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuingia katika mizozo na waamuzi, kwani Novemba mwaka jana mwenyekiti wao Ibrahim Haciosmanoglu alifungiwa siku 280 baada ya kuwafungia waamuzi wanne uwanjani kwa kushindwa kutoa penati kwa timu hiyo.
#Source_bbc_sport