Kufuatia kuwepo kwa uchafu ulio kithiri ndani ya Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma watu wawili wameripotiwa kufariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huku wengine 28 wakigundulika kuugua ugonywa huo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa huo Daktari Fadhiili Kibaya ambaye amesema kuwa maeneo ambayo yamebainika kuathiriwa sana ni pamoja na Kata ya Kibirizi na mpaka sasa Manispaa kwa kushirikiana na Ofisi za afya mkoa tayari wameanza hatua za awali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.
"Baada ya vipimo kufanyika ndipo Ikagundulika kuwa watu hao wawili waliofariki wamekufa kwa ugonywa wa kupindupindu huku kukiwa na wagonjwa 28 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Kikunku" Amesema Dkt. Fadhiri.
Aidha Dkt. Fadhili amewasihi wakazi wote wa mkoani Kigoma kuimarisha usafi kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuzingatia kwanini za usafiri ikiwemo kuepuka kunywa maji yasiyochemshwa lakini pia kuepuka kula Kinyesi kwa kunawa mikono mara tu baada ya kutoka chooni sambamba na kuzingatia matumizi sahihi ya vyoo.
Hata hivyo wakazi mkoani humo wametakiwa kuripoti mara moja kwenye vituo vya afya mara watakapobaini dalili za ugonjwa huo ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza.