Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Sep 13, 2017

MGOGORO WAIBUKA BAINA YA SERIKALI NA WANANCHI KIGOMA

Wakati mvutano ukiendelea baina ya serikali na wakazi wa pembezoni mwa barabara inayojengwa ya kasulu kidahwe Mkoani Kigoma kuhusu mahali pa kuchimba vifusi kwa ajiri ya barabara hiyo, Serikiali imeshauliwa kumaliza changamoto hiyo ili kuendelea na ujenzi.

Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Muguha Titus Muguha ameeleza katika baraza la madiwani la kufunga robo ya mwaka lilofanyika hivi karibuni huku akiongeza kuwa, kuna haja ya kutatua changamoto ndogo ndogo za migogoro ili kufanya shughuli kwa amani.

Amesema viongozi hawatakiwi kuwa sehem ya kuchochea migogoro ya aina yoyote bali wanatakiwa kuwa mstali wa mbele kutatua migogoro hiyo.

Aidha Bw, Titus amesema kuwa halmashauri inapaswa kutenga mipaka ya ardhi inayomilikiwa na serikali pamoja na jamii, jambo litakalo epusha kuvamia maeneo ya umma.

Hatahivyo baadhi ya madiwani wa kata za halmashauri ya mji wa kasulu wameunga mkono suala hilo nakusema, nivema hatua zianze kuchukuliwa mapema iwezekanavyo ikiwa nisehem ya kuweka mahusiano mazuri kati ya serikali wana jamii.