Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Sep 12, 2017

WAZIRI AAGIZA VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI KUJENGWA MKOANI KIGOMA

Serikali mkoani Kigoma Imetakiwa kuanza miradi ya ujenzi wa Zahanati katika kila kijiji na Vituo vya afya kwenye kila kata sambamba na kukamilisha majengo yaliyojenga na wananchi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Daktari Hamis Kigwangala ameyasema hayo hivi karibuni Katika kijiji cha Mwakizega Kata ya Mwakizega Wialaya ya Uvinza mkoani hapa, wakati akifungua mradi wa majengo 26 ya kutolea huduma za afya ya mama na mtoto majengo yanayojengwa kwa udhamini wa shirika la Ingender Hearth.

Amesema licha ya kujengewa vituo 26 katika vijiji tofauti mkoani hapa lakini bado kuna uhitaji wa vituo vya afya na zahanati kutokana na mahitaji ya wananchi waishio vijijini,  na amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa wananchi pale wanapoanza kujengo vituo hivyo.

Aidha kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmanuel Maganga amesema mkoa umepiga hatua kutokana na msaada wa majengo hayo 26 yatakayotoa huduma za afya na sambamba na kuahidi kuyatumia majengo hayo kwa manufaa ya wananchi na amewataka wananchi kuyatunza kwa ajiri ya manufaa ya afya zao.

Kwa Upande wake  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Daktari Fadhiri Kibaya, amesema mkoa una jumla ya Vituo vya kutolea huduma za afya 278 huku mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi MAM ni kuwa na Zahanati katika kila kijiji na Kituo cha afya kwa kila kata huku akibainisha kuwa changamoto inayoikabiri sekta ya Afya mkoani hapa ni Kukosekana kwa watumishi pia bado kuna uhitaji wa zahanati na vituo vya afya.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Engender Hearth Tanzania Lulu Ngwanakilala amesema shirika hilo limeweka kipaumbele katika kuleta mabadiriko ya kudumu hususa ni katika afya ya jamii huku akibainisha kuwa gharama iliyotumika katika ujenzi wa majengo hayo ni shilingi bilioni 2.75.