Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Sep 17, 2017

MOTO WATEKETEZA NYUMBA YA MBUNGE ZITTO KAMBWE

Nyumba ya Mbunge wa Kigoma Mjini Muheshimiwa Zitto Zuberi Kamwe iliyopo Kibingo mji mdogo wa Mwandiga barabara ya kuelekea Manyovu imeteketea kwa moto baada ya kutokea kwa hitirafu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Naibu Kamishina Ferdinand Mtui hii leo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Siku ya Jana septemba 16 majira ya saa 10:40 jioni na kuteketeza nyumba hiyo na mali zote zilizokuwemo ndani.

Aidha Kamanda Mtui ameongeza kuwa Nyumba iliyoungua ni ndogo ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa Mbunge huyo na Kama inavyofahamika Mbunge huyo ana nyumba Mbili eneo hilo.

"Vitu vilivyoteketea ni Pamoja na vitanda vitatu, godoro moja, seti moja ya sofa, mota ya kupandishia maji, zulia moja, panel sita za solar, Berri nne na vitu vingine vidogo vidogo " amebainisha Kamanda Mtui .

Hata hivyo Kamanda Mtui amesema chanzo cha MOTO huo ni betri ya umeme wa jua kuzidiwa nguvu kisha kulipuka na kusababisha moto ulioteketeza nyumba yote.