Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Sep 9, 2017

SERIKALI YACHUKUA HATUA BAADA YA MACHINJIO YA KIBIRIZI KIGOMA KUFUNGWA

Baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kanda ya magharibi kufunga machinjio ya kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji, serikali ya Manispaa hiyo imeanza mikakati ya ukarabati wa machinjio hiyo ili kuendelea kutoa huduma kwa jamii.

Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw.Bennet Ninalo amekiri kuwepo kwa uchakavu wa machinjio na kusema ukosefu wa fedha kutoka serikalini ndiyo chazo kikubwa cha machinjio hiyo kufungwa kwa kukosa vigezo vinavyokidhi.

Aidha Ninalo amesema manispaa yake tayari imeanza juhudi za ukarabati wa machinjio hiyo kwa bajeti ya mwaka 2017/ 2018 ili wakazi wa manispaa hii waendelee kupata huduma hiyo.