Waziri wa maji na Umwagiliaji Muhandisi Isack Kamwene amemtaka mkandarasi anayesimamia mradi wa maji Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda alioutoa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli.
Ziara ya waziri wa maji na Umwagiliaji muhandisi Isack Kamwene imetembelea miradi mbalimbali mkoani hapa ukiwemo ule wa Bangwe ambapo katika ziara yake amebaini hatua mbalimbali ambazo mradi huo umefikia.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo waziri amesema hawezi kukubali kuona Rais anadanganywa na badala yake hatua kali zitachukuliwa endapo mradi huo hautakamilika ndani ya muda ulikusudiwa ambao ni nov 30 mwaka huu.
Aidha katika hatua nyingine waziri Kamwene amesema kuna tatizo ambalo amelibaini baada ya kusikiliza maelezo ya mkandarasi juu ya baadhi ya vifaa vilivyoagizwa kuchelewa kufika na kusema anachopaswa kufanya ni kuhakikisha angalau baadhi ya wakazi wanaanza kupata maji.
Hata hivyo waziri huyo amesema agizo la Raisi limelenga kuhakikisha maji yanatoka katika maeneo yote yaliyokusudiwa na sivinginevyo.
Zikiwa zimesalia taribaani siku 24 katika maelekezo ya Raisi John Pombe Magufuri wakati wa ziara yake mkoani hapa na kazi ikiwa bado inaendelea imeelezwa kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 78 hali inayoleta matumaini kwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.