Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 20, 2017

IGP SIRRO AMPANDISHA CHEO ASKARI WA KIKE KIGOMA

Mkuu wa jeshi  la polisi nchini IGP Simon Sirro  amempandisha cheo askari wa jeshi hilo kikosi cha Kutuliza ghasia FFU mkoani Kigoma Tamal Moses baada ya askari huyo kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika onyesho la gwaride  la uhodari wakati wa ziara yake mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kumvisha Cheo hicho kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi nchini kamanda wa jeshi hilo  mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi Martin Ottieno amesema Tamal  amepandishwa cheo kutoka ngazi ya  Copro  hadi sajini wa polisi.

Kwa upande wake Tamal Moses aliyepandishwa cheo ameushukuru uongozi wa mkoa kwa ujumla huku akiahidi kuongeza juhudu katika kazi ili kufika mbele zaidi.

Hata hivyo IGP Sirro amefanya ziara yake mkoani  Kigoma hivi karibuni  ikiwa ni hatua ya kuimarisha utendaji wa jeshi hilo katika kusimamia sheria kwa maendeleoo na usalama wa nchi.