Baada ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu mkononi Kigoma ambapo hadi sasa watu 6 wamepoteza maisha na wengine 156 kuugua ugonywa huo, Mganga mkuu wa mkoa huo amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia Kanuni za afya hasa wilaya za Kigoma na Uvinza ambazo mara nyingi ugonjwa huo huanzia huko.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Daktari Paul Chaote, mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa yenye changamoto ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindu pindu kila mwaka na hasa misimu ya mvua hali ambayo imeelezwa ni kutokana na baadhi ya wananchi kutozingatia masuala ya afya ikiwemo ukosefu wa vyoo kwenye makazi yao , kutumia maji ambayo hayajachemshwa na wengine kufua nguo kwenye maeneo ya mwambao wa ziwa Tanganyika.
Aidha Daktari Chaote ameongeza kuwa hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa wahudumu wa afya katika makazi ya waathirika wa mlipuko ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Hata hivyo dr Chaote ametoa wito kwa wakazi mkoani hapa kuzingatia matumizi sahihi ya vyoo ikiwa ni pamoja na kusitisha kutumia maji ya mto hadi pale ugojwa huo utakapotoweka.