Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Mar 21, 2018

HUMPHREY POLEPOLE APINGWA NA SERIKALI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI

Katibu mwenezi wa CCM Humphrey Polepole 

Manispaa ya Kigoma ujiji imesema itaendelea kusimamia sheria ndogo mpya iliyosainiwa na Ras kupitia TAMISEMI 2017, Sheria ya  kodi ya vibanda shilingi elfu 50 licha ya Jumapili iliyopita Katibu mwenezi wa CCM Humphrey Polepole kueleza kufuta sheria hiyo nakuwatangazia wafanyabiashara wa Kigoma mjini kuendelea na kodi ya zamani  ya elfu 15.

Mstahiki Meya wa Manispaa hii Husen Ruhava ameyasema hayo akiwa ofisini kwake nakwamba anaamini kinachofanywa na kiongozi wa CCM wa ngazi ya juu ni siasa kwasababu maelekzo ya kiserikali hayawezi kupitia kwenye chama.

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussen Ruhava
Meya amewataka watendaji katika ngazi ya manispa wanaohusika na ukusanyaji wa kodi hiyo kutoyumba na badala yake waendelee kukusanya kiasi cha elfu hamsini hadi hapo barua rasmi ya Rais itakapoifika manispaa

Hata Hivyo wanyabiashasha katika manisapaa hii kupitia mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiashara mkoa, Juma Chaurembo wamefurahishwa na ufutwaji wa kodi hiyo, huku wakisema  watafuta shauri walilofungua mahakamani kuhusu kadhia hiyo.

Jumapili  machi 18 Humphrey Polepole amesema hatua ya kufuta kodi hiyo nikutokana na kuwa kubwa ikipingana na sera ya chama nakwamba ni baada ya kuwasiliana na mamlaka zote za juu za serikali ikiwemo Rais Dk John Pombe Magufuli.