Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wamefariki dunia huku watatu wakitokomea kusiko julikana baada ya shambulizi baina ya majambazi hao na Askari polisi katika eneo la Makere wilayani Kasulu ambapo katika tukio hilo askari mmoja amejruhiwa mkono.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa Kamishina Msaidizi Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea March 19 lililowahusisha Bukuru Steven ambaye ni mkimbizi na Nobart Andrew wakiwa wanamiliki silaha mbili aina ya AK 47 zikiwa na jumla ya risasi 41.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda Otieno amesema baada ya kuwakamata majambazi hao walikiri makosa na kwenda na polisi kwa lengo la kuwaonyesha siraha walizoficha sambamba na wenzao
Wakati wakielekea katika poli zilipofichwa siraha hizo ghafla majambazi wengine waliokuwa wamejificha walianza kurusha risasi mfululizo ambazo kwa bahati mbaya ziliwapata majambazi wale wawili waliokuwa na polisi na kufariki dunia huu askali mmoja akipigwa risasi ya mkono amesema Kamanda Otieno.
Hata hivyo kutokana na kushamiri kwa matukio ya unyanganyi na ujambazi wa kutumia silaha, Kamanda Otieno ametoa siku 30 kwa wakimbizi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa jeshi la polisi na kuongeza kuwa kutafanyika oparesheni kubwa katika kambi zote za wakimbizi mkoani hapa.