Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Mar 7, 2018

KABOUROU KUZIKWA KIGOMA IJUMAA

Aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kigoma Dk. Amani Walid Kabourou aliyefariki usiku wa kuamkia leo, atazikwa Ijumaa Machi 9, mwaka huu mkoani humo.

Kwa sasa mipango ya mazishi na kusafirisha mwili huo inaendelea nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa familia, Hasna Mwilima, amesema mwili wa marehemu Dk. Kabourou utasafirishwa kesho kuelekea mkoani Kigoma ambapo atazikwa katika makaburi ya Kipampa, Shule ya Ujiji mkoani humo.

“Tumekosa usafiri wa ndege kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu hivyo inatulazimu kuzika ijumaa kwa sababu tutatumia usafiri wa barabara.

“Hii ni kwa sababu kuna msiba mwingine ambao utasafirishwa kwa ndege wenzetu hao waliwahi kufanya ‘booking’ mapema,” amesema Hasna.

Dk. Kabourou alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili mauti yalipomkuta.

Source: Mtanzania