CHAMA
cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma (KGPC) kimepata viongozi wapya watakao
kiongoza chama hicho kwa miaka mitatu, baaada ya viongozi wa awali kumaliza
muda wao.
Viongozi
hao walichaguliwa hapo janakatika
Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho na kuunda baraza litakalokiongoza chama
hicho kwa muda wa miaka mitatu kama isemavyo kanuni ya Umoja wa Vyama vya
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Katika
Uchaguzi huo uliosimamiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kividea, Babu Paschal, ulishuhudia
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika chama hicho ambaye ni mwakilishi wa
ITV/Radio One Deoclatius Nsokoro akichaguliwa tena kukiongoza chama hicho.
Aidha,
wanachama wa KGPC walimchagua Adera Madyane kuwa Mwenyekiti Msaidizi, nafasi ya
Katibu Mkuu ikachukuliwa na Mwakilishi wa Gazeti la Habari Leo Fadhiri Abdalah
huku nafasi ya Katibu Msaidizi akichaguliwa Mwakilishi wa Clouds FM na Gazeti
la Nipashe Emmanuel Johnson Matinde.
Kwa
upande wa nafasi ya Muhasibu wanachama walimchagua Mwajabu Kigaza na
waliochaguliwa katika Nafasi ya Ujumbe wa Kamati Tendaji walikuwa ni Winfrida
Bwire, Emmanuel Senny, Kassimu Msoma na Prosper Kwigize aliyeteuliwa na
mwenyekiti.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Kigoma (KGPC) Deoclatius Nsokoro ambaye ni mwakilishi wa ITV na Radio One, akitoa shukrani zake baada ya kuchaguliwa tena kukiongoza chama hicho
Mwenyekiti msaidizi wa KGPC akiwashukuru waandishi wa habari kwa kumchagua katika nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Katibu mkuu wa KGPC ambaye ni mwandishi wa gazeti la Habari, Fadhiri Abdalah akitoa shukrani zake baada ya kuchaguliwa
Mwakilishi wa Channel Ten, Jacob Ruvilo aliyekuwa Katibu Mkuu wa KGPC akiwashukuru kuwaaga wanachama baada ya kutangaza kutokugombea tena.
Katibu Msaidizi wa KGPC Emmanuel Johnson Matinde ambaye ni mwakirishi wa Clouds FM na gazeti la Nipashe , akitoa shukrani zake kwa wanachama baada ya kuchaguliwa.
Mwandishi wa Gazeti la Kigoma Yetu, Winfrida Bwire, akitoa shukrani zake kwa wanachama baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa kamati Tendaji.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima Emmanuel Senny akitoa shukrani zake kwa wanachama baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa kamati Tendaji KGPC.
Mpiga Picha wa ITV Kassimu Msoma akitoa shukrani zake kwa wanachama baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa kamati Tendaji KGPC.
Mwakilishi wa BBC Prosper Kweigize, akitoa shukrani zake kwa wanachama baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati Tendaji.