Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 7, 2015

KOEMAN: SCHNEIDERLIN ATAJIUNGA MAN UNITED KAMA WAKILIPA PESA YA THAMANI YAKE

Kocha wa klabu ya Southampton, Ronard Koeman ameiambia timu ya Manchester united kama inamtaka mchezaji wa timu hiyo Morgan Schneiderlin inapaswa kutoa pesa inayoendana na mchezaji huyo.

Koeman amesema kwa timu kama Manchester united pesa kwao siyo shida na hivyo wanatakiwa kuongeza pesa ili wampate Schneiderlin.

Amesema kuwa wiki Mbili zilizopita walipokea ofa kutoka Manchester united lakini haikuwa na thamani ya kutosha.

Koeman ameongeza kuwa Schneiderlin ni moja kati ya wachezaji muhimu katika timu yake nani mchezaji wa kimataifa hivyo kwa timu inayohitaji huduma yake inapaswa kutoa ofa kubwa itakayoweza kuwashawishi kumwachia mchezaji huyo.

Wiki Mbili zilizopita Manchester united ilituma ofa ya Paundi millions 20 lakini ilikataliwa na taarifa zinasema kuwa Manchester united inajipanga kutoa ofa ya Paundi millions 30.