BAADA ya aliyekuwa mgombea ubunge
katika jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kufungua kesi ya kupinga matokeo
yaliyompa ushindi mgombea wa CCM Hasna Mwilima, Kesi hiyo imeahirishwa mpaka
jumatatu Novemba 30-2015.
Kesi hiyo iliyopewa No. 2/2015
ilitarajiwa kusikilizwa leo hii katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora ambapo Jaji
wa Mahakama hiyo, Mhe Utamwa aliamua kuahilisha kesi hiyo kwa hoja kwamba mshtakiwa wa kwanza Bi Husna
Mwilima anapaswa kujibu kwanza kabla kesi haijaendelea kusikilizwa na
kuamuliwa.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo
ni Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya Uvinza Eng. Lubeni Mfune, pamoja na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.
Jaji Utamwa ameagiza kesi hiyo kusikilizwa jumatatu ili kuendana na muda
uliopo kisheria ambapo kesi hii ndogo inapaswa kuamuliwa ndani ya siku14 ili
kesi ya msingi iweze kuendelea.
Katika kesi hii ndogo ya awali kabla
ya kesi ya msingi, mahakama itaamua kiasi ambacho Mh Kafulila atatakiwa kulipa
kama gharama za dhamana ambayo kisheria kwa wastakiwa watatu wanatakiwa kulipa
Tsh. milioni15.
Madai ya Kafulila katika kesi hiyo, anamlalamikia
msimamizi wa uchaguzi kwa kumtangaza mgombea ambaye hakustahiri kutangazwa mana
hakupata kura nyingi ila inadaiwa alifanya hivyo kwa shinikizo kutoka ngazi za
juu serikalini.