Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Nov 27, 2015

MTOTO WA MIAKA 5 AFARIKI BAADA YA KUBAKWA KIGOMA



MTOTO mmoja ajulikanae kwa jina la Anna Kabembo (Sio jina lake kamili)  mwenye miaka mitano na mkazi wa kijiji cha Katuguru Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya kubakwa na watu wasiojulikana.

Akizungumza na Waandishi wa habari hapo jana, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui alisema kuwa, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9:30 arasili katika kijiji cha Katuguru wakati mtoto huyo akicheza na wenzake.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui akizungumzia tukio la mtoto kubakwa.

Kamanda Mtui alisema kuwa, wakati watuhiwa wakifanya kitendo hicho mtoto yule alikuwa akipiga kelele hivyo watuhumiwa wakaamua kumziba pua na mdomo jambo lililopelekea kukosa pumzi na kufariki.

“Katika eneo la tukio kulikuwa ni mita 200 kutoka nyumbani kwao  mpaka mwili ulipokutwa  na inavyoonekana sehemu alipofanyiwa kitendo hicho ni kwenye nyumba yenye uzioa mana kutoka kwenye hiyo nyumba kulikuwa na mibuluzo ya miguu hadi ulipokuwa mwili kitu kinachofanya tuamini kuwa baada ya kumbaka walimbuluza mpaka nje” alisema Kamanda Mtui.

Aidha Kamanda Mtui alisema kuwa,  Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo Kamanda Mtui aliwataka wazazi kuwa makini wanapowaacha watoto wao nyumbani kwa kuwaacha chini ya uangalizi wa watu wakubwa ili kuepusha kutokea kwa matukio kama haya.

“Wazazi wa mtoto huyo waliondoka asubuhi kwenda kwenye shughuri zao na kumuacha mtoto akicheza na wenzake lakini hakuna mtoto yule alichukuliwaje na watuhumiwa na hata wale watoto wenzake hawajui chochote, Wazazi walitakiwa kujua wanamuacha mtoto wao katika mazingira gani” aliongeza Kamanda Mtui.