BAADA
ya zoezi la uandikishaji wa Raia wa kigeni nchini kukwama, Uhamia Mkoa wa
Kigoma imewataka raia hao kutokupuuza zoezi hilo kwani litaendelea baada ya
kutatua chamngamoto zilizojitokeza awali.
Mmoja wa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na familia yake wakiwa wameshika CARD walizopewa baada ya kuandikishwa katika hatua ya kwanza ya zoezi hilo |
Akizungumza
na Blog hii Ofisini kwake, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Naibu Kamishina Maurice Kitinusa, alisema kuwa, zoezi la
uandikishaji wa raia walowezi lilitakiwa kufanyika katika wilaya zote za mkoa
huu lakini kutokana na changamoto zilizokuwa nje ya uwezo zoezi hilo lilikwama
katika hatua ya kwanza tu.
Alisema
kuwa, zoezi hilo lina hatua tatu ambapo lilikwama katika hatua ya kwanza na
hatua hiyo ilikamilika katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Kigoma vijini na baadhi
ya vijiji katika wilaya ya Uvinza kwahiyo wilaya za Kasulu na Kibondo zoezi
hilo lilikuwa bado halijaanza.
Afisa uhamiaji mkoani Kigoma akiendelea na zoezi la uandikishaji wa Raia walowezi katika hatua ya kwanza ya zoezi hilo kabla ya kusitishwa |
“Kwahiyo
tumeshindwa kuendelea na hatua zinazofuata kwasababu hata hatua ya kwanza bado haijakamilika
na kwa wilaya zingine haijaanza kabisa endapo tungekuwa tumeshakamilisha hatua
ya kwanza sasahivi tungekuwa tupo kwenye hatua ya pili au ya tatu” alisema
Kitinusa
Aidha
Kitinusa aliwataka raia wote walowezi kuwa na
subira mana zoezi hilo litaendelea kwa hatua zilizobaki na kwa wilaya
ambazo lilikuwa halijaanza litaanza ili kufikia malengo na muda wa kuanza
upya matangazo yatatolewa ili raia wote
wawe na taarifa.
Akizungumzia
Changamoto zilizosababisha zoezi hilo kukwamba Kitinusa alisema kuwa,
kukosekana kwa Pesa za kutosha, uchache wa Maafisa uhamiaji na vitendea kazi
kama magari ndio kulisbabisha zoezi kukwama.
“Mkoa
ni mkubwa na kuna viijiji ambavyo havifikiki kirahisi hivyo magari yanatakiwa
ya kutosha pia ni lazima kuwepo na maafisa uhamiaji wakutosha ili kuwatawanya
maeneo yote” alisema Kitinusa.
Kitinusa
aliongeza kuwa, kwasasa wanasubiri serikali ikae na wafadhiri wa zoezi hili
ambao ni IOM ili kupanga kuanza upya zoezi hilo na kushughurikia changamoto
zilizosababisha zoezi la awali kukwama ili zoezi likianza lisikwame tena.
Hata
hivyo Kitinusa, aliwataka raia walowezi ambao wameshakamilisha zoezi katika
hatua ya kwanza watunze kadi walizopewa na maafisa uhamiaji ili
zoezi likianza upya iwe rahisi kwao kuendelea na hatua zinazofuata pia baada ya
kukamilika kwa zoezi raia wote ambao walipuuzia zoezi hilo hawatoruhusiwa
kuendelea kuishi nchini.
"Kadi zile ni za muhimu sana pia inamfanya mtu aendelee kuishi nchini kwa kutumia hizo kadi wakati akisubiri hatua zingine zilizobaki katika zoezi zima" alisema Kitinusa.
"Kadi zile ni za muhimu sana pia inamfanya mtu aendelee kuishi nchini kwa kutumia hizo kadi wakati akisubiri hatua zingine zilizobaki katika zoezi zima" alisema Kitinusa.
CARD zilizokuwa zikitolewa na Uhamiaji baada ya kuandikishwa katika hatua ya kwanza ya zoezi hilo |
Awali
wakizungumzia kukwama kwa zoezi hilo raia wa walowezi mkoani hapa, walisema
kuwa wakati zoezi hilo linaanza liliwapa matumaini ya kuishi nchini kwa amani
na wengine kurudi katika nchi zao ila baada ya kukwama wanashindwa kuelewa nini
hatima yao.
John
Bigilimana kuoka nchini Burundi alisema kuwa baada ya kuambiwa maelengo ya
zoezi hilo aliamua baada ya kukamilika arudishwe nchini kwao ili akaanze maisha
mapya katika nchi yake badara ya kukaa ugenini ila baada ya kukwama haelewi
nini kitakachofuata baadae
Asajile
Hamisi ambaye ni raia wa Congo alisema kuwa, suala linalowachanganya ni zoezi
kukwama bila kuambiwa ni kama litaendelea au la na akaomba serikali
iwafahamishe kama zoezi lipo au halipo ili wajue kuliko kusubiri kitu ambacho
kakipo.
Baadhi ya raia kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu waliokuwa wakiishi bila vibali mkoani Kigoma waliokuwa wamejitokeza kuandikishwa katika zoezi la uandikishaji hatua ya kwanza kabla ya kukwama. |
“Mimi
kwa upande wangu niko na ndungu zangu watatu na wote tumeshakamilisha hatua ya
kwanza na vyetu tulivyopewa tunavyompaka
sasa pia maazimiao yetu ni kuwa raia wa Tanzania mara baada ya zoezi kukamilika
mana shughuri zetu zote tunazifanyia huku hatuoni haja ya kurudi Congo tukawe
maskini, hivyo tunaomba serikali itwambie kama tuendelee kusubiri au la”
alisema Asajile.
Baadhi ya raia kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu waliokuwa wakiishi bila vibali mkoani Kigoma waliokuwa wamejitokeza kuandikishwa katika zoezi la uandikishaji hatua ya kwanza kabla ya kukwama |