WAKATI Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) ukiendela na zoezi lake la ugawaji wa pesa ili kunusulu kaya maskini
kwa awamu ya tatu katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Wananchi katika
Wilaya hiyo wametakiwa kutimiza masharti ili kutimiza malengo ya mfuko huo.
Mfuko huo unalenga kwa kila kaya
inayopewa msaada kuhakikisha inazitumia pesa hizo kuwapeleka watoto shuleni
sambamba na akina mama kuhudhulia klini kwa asilimia 80.
Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Simoni Mumbeye wakati akizungumza na Wananchi
wa Kijiji cha Msagala Wilayani humo ambapo alisema kuwa, Serikali kupitia
TASAF awamu ya tatu inahitaji kuziwezesha kaya maskini ili kukidhi mahitaji ya
elimu kwa watoto pamoja na akina mama wajawazito wanaotakiwa kwenda kliniki.
Wananchi wanaotoka katika kaya maskini wakigawiwa pesa katika zoezi linalofanywa na TASAF awamu ya Tatu. |
Alisema kuwa, serikali inahitaji
kuona hakuna kaya ambayo inashindwa kuwapeleka watoto shuleni kwasababu ya
kukosa pesa sambamba na akina mama kushindwa kufika klini mara wanapohitajika
kufanya hivyo.
“Kinachotakiwa kufanyika kwa
wananchi ambao wameshapewa pesa ni kutimiza maagizo hayo na si vinginevyo kama
ni watoto walikuwa hawaendi shule basi wapelekwe mara moja mana ndio lengo la
TASAF” alisema Mumbeye.
Aidha Mumbeye alisema kuwa, endapo kuka kaya itabainika inatumia pesa
hizo kwa shughuri zingine tofauti na maelekezo ya TASAF, kaya hiyo itatolewa
katika orodha na nafasi yake itapewa kaya nyingine yenye sifa.
“Wengine baada ya kupewa pesa hizo
huzitumia kwa kunywa pombe au kuzitumia katika njia ambazo hazina faida kwa
familia, lakini naomba mtambue kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo
ya TASAF” alisisitiza Mumbeye.
Kwa mujibu wa Mratibu wa TASAF wilayani
humo, Deogratiasi Chubwa, jumla ya shilingi milioni 960 zilitolewa kusaidia
kaya masikini katika vijiji 36 ambapo kaya elfu 8932 zilinufaika wilani hapo.
Kwa upande wao baadhi ya walengwa
walionufaika na mradi huo Agripina Dagrasi na Ezekia Mfaume walisema kuwa baada
ya kupokea pesa kutoka TASAF tayari wanaona mabadiriko katika familia zao kwani
watoto wao kwasasa wanakwenda shule pia pesa hizo zinawasaidia katika mahitaji
madogomadogo ya kifamilia.
Wananchi wanaotoka katika kaya maskini wakigawiwa pesa katika zoezi linalofanywa na TASAF awamu ya Tatu. |