JESHI
la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Meshack Mtondo (37) mkazi wa Kijiji cha Kasanda Katika Wilaya ya
Kakonko mkoani Kigoma kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya tembo pamoja na
risasi 32 za SMG ambacho ni kinyume na sheria.
Akizungumza na Blog hii leo leo hii, Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Ferdinand
Mtui, alisema kuwa, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya
7:00 mchana baada ya askari kupata
taarifa kutoka kwa wasamalia wema.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui akionyesha meno ya tembo yaliyokamatwa. |
Alisema
kuwa, baada ya Polisi kupewa taarifa walifika nyumbani kwa mtuhumiwa na
walipofanya upekuzi walifanikiwa kukamata meno mawili ya tembo pamoja na risasi
32 vyote vikiwa ndani ya mfuko wa sandarusi.
“Juhudi
za kukamatwa kwa mtuhumiwa zilichangiwa na wananchi wanaochukia uharifu ambao
baada ya kubaini umilikwaji wa nyara hizo za serikali walitoa taarifa kwa
Polisi waliokuwa doria na kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa” alisema kamanda
Mtui.
Risasi 32zilizokamatwa nyumbani kwa Meshack Mtunda. |
Aidha
Kamanda Mtui alisema kuwa, Mtuhumiwa alikamatwa na taratibu za kumfikisha
mahakamani zinaendelea ili akajibu mashitaka yake ya kumiriki Nyara za serikali
ambacho ni kiyume na sheria pamoja risasi zile.
Hata
hivyo Kamanda Mtui aliwapongeza wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha ambao
ulipelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa pia aliwataka wananchi kuendelea kutoa
taarifa kwa Polisi kila wanapobaini vitendo vya kiharifu.