WAFANYABIASHARA mkoani Kigoma
wamelitaka shirika la Bima ya Afya (NHIF) kuwarekebishia masharti ya kujiunga
na mfuko huo kama ilivyo kwa wananchi walioko kwenye Taasisi na makundi
mbalimbali.
Hayo yalizungumzwa katika mkutano kati
ya wafanyabiashara na NHIF mkoani hapa, ambapo wafanyabiashara hao waliomba
taratibu iliyowekwa ya kila mfanyabiashara kulipia kiasi cha Tshs 76000 bila
kuwa na mtu hata mmoja ndani ya familia ibadilishwe ili na wao wajiunge katika
mfuko huo.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kigoma, akitoa mada katika semina kati ya NHIF na Wanyabiashara. |
Akitoa maoni kwa niaba ya
wafanyabiashara, Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara (TCCIA) mkoani
Kigoma, Sethi Naftari, alisema kuwa NHIF ilitoa kipaumbele kwa wananchi
walioajiliwa na walioko katika makundi mbalimbali kujiunga katika mfuko huo kwa
Tshs 76000 huku wakiwajumuisha wategemezi wao katika familia.
Alisema, kwakuwa mfuko huo una lengo
la kuwasaidia watanzania wote unatakiwa kuregeza masharti kwa wafanyabiashara
ambao wamejiajiri wenyewe ili nao waweze kujiunga katika mfuko huo na kunufaika
na matibabu pamoja na wategemezi wao katika familia.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Mkoa wa Kigoma, Sethi Naftari, akitoa maoni kwa niaba ya wafanyabiashara. |
"Ni kweli wengi wetu tulikuwa
hatuna uelewa kuhusu faida za Bima ya Afya ila baada ya NHIF ktoa elimu sote
tumeelimika na tunakiu ya kujiunga mana sula magonjwa halikwepeki lakini ni
vyema wakalekebisha masharti yao kwetu wafanyabiashara " alisema Naftari.
Nao baadhi ya wafanyabiasha akiwemo
Idd Kimenyi, Frola Jonathan na Michael Sabwebwe, walisema kuwa, elimu
waliyoipata ni nzuri lakini tatizo ni upande wa malipo ya kujiunga na mfuko huo
ambayo yanamfunga mfanyabiashara kujiunga na mfuko huo akiwa peke yake licha ya kuwa ana familia.
Walisema Kuwa ili kuweka usawa kwa
lengo la kuwasaidia watanzania wote ni vyema taratibu hiyo ikabadirishwa kwa
watu wote bila kubagua ili na watu wao waweze kumudu gharama hiyo ambayo
itawasaidia pamoja na wategemezi wao.
“Mimi nina mke na watoto lakini NHIF inasema
natakiwa kujiunga peke yangu tena kwa pesa nyingi jambo ambalo linakuwa ngumu
kwangu, sasa kama wa wanahitaji kutusaidia basi wapunguze ada ya kujiunga iwe
chini ya Tsh. 76000 au waache hiyo hiyo lakini watuache tuwajumuishe wategemezi
wetu katika familia kama ilivyo kwa waajiriwa na watu kutoka makundi
mbalimbali” alisema mmoja Michael Sabwebwe.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa NHIF
mkoani Kigoma, Emmanuel Antony alisema kuwa kwasasa wanatoa elimu katika
makundi mbalimbali kufahamu faida za mfuko wa Bima ya Afya ndio mana waliamua
kuongea na wafanyabiashara.
Alisema kuwa, kwa wale ambao
wameelewa umuhimu wa kuwa na uhakika wa matibabu muda wowote hawatojari gharama
ya kujiunga kwani suala la kuugua ni la kila mtu na mtu anaweza kuugua Muda
wowote hivyo kama ana Bima ya Afya atatibiwa bure hata kama ugonjwa wake
unagharimu pesa nyingi hadi kupona.
Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kigoma walioshiriki katika mkutano kati ya NHIF na wafanyabiashara kwa lengo la kupata elimu. |
Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kigoma walioshiriki katika mkutano kati ya NHIF na wafanyabiashara kwa lengo la kupata elimu. |