Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 18, 2015

SIRI YA MAFANIKIO: NYIMBO INAYOKONGA NYOYO

Msanii wa nyimbo za injili anayechipukia hapa nchini Tanzania  Alfa Obed Luziro amesema moja kati ya nyimbo aliyoitoa hivi karibuni imeonekana kupendwa na kuwakonga nyoyo wapenzi na mashabiki wa nyimbo hizo.

Akizungumza na Blog hili msanii huyo anayefanya vizuri katika uimbaji wake amesema, nyimbo hiyo inayoitwa Siri ya Mafanikio ambayo bado video yake inaendelea kuandaliwa imeonekana kupendwa zaidi na wapenzi wa music wa nyimbo za injili na wasiokuwa wapenzi wa nyimbo hizo kutokana na utunzi wake pamoja na ujumbe ulioko ndani yake.
Mwimbaji wa nyimbo za injili Alfa Obed Luziro
Alfa ambaye tayari ametoa album yake ya audio na video inayojulikana kwa jina la YESU NI MCHUNGAJI MWEMA ambayo kwa sasa iko sokoni wakati kazi hiyo ikiendelea kufanya vizuri anajipanga kuhaikisha album ya video anayoitoa awamu hii inakuwa kali zaidi kuliko ya mwanzo.


‘‘Album yangu ya kwanza inayoitwa Yesu ni mchungaji Mwema imefanya vizuri na kunitambulisha katika music wa kiinjili na sasa hivi niko jikoni nikipika kitu kingine kipya ambacho kitakuwa kikali zaidi’’ alisema msanii huyo.

Akizungumzia kazi zake kwa sasa msanii huyo amesema amekuwa akipata mialiko mingi ya kushiriki matamasha mbalimbali na mikutano ya nje na ndani ya wilaya yake ya Kasulu anayoishi kutokana na kazi yake kuwafikia wengi kupitia katika vyombo vya habari.

‘‘Nyimbo zangu. zinapigwa maeneo mbalimbali namshukuru Mungu kusema ukweli, radio zimekuwa msaada mkubwa kwangu mfano radio kwizera, TBC kigoma na nyingine nyingi zimekuwa zikicheza nyimbo zangu nah ii imenifanya kufahamika maeneo mbalimbali na hivi sasa mialiko ya kwenda kutoa huduma katika makanisa na mikutano mbalimbali imekuwa kubwa’’ alisema msanii huyo

Hata hivyo Alfa amesema licha ya band yake inayoitwa ALFA OBED LUZIRO GOSPAL BAND kufanya vizuri bado anakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa wadhamini wa kusaidia kuinua wasani wachanga ili kufanya kazi nzuri zaidi.