Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 5, 2016

LEICESTER CITY YAPATA PIGO BAADA YA VARDY KUUMIA

Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy (kulia) akishangilia moja ya mabao yake sambamba na mchezaji mwenzake Mihrez
Klabu ya Leicester City imepata pigo baada ya kufahamika kuwa mshambuliaji wake tegemeo Jamie Vardy hataweza kucheza kwa wiki mbili baada ya kufanyiwa upasuaji.

Vardy ambaye ni raia wa Uingereza amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye mtoki wake, kituo cha redio cha BBC cha Leicester kimeripoti.

Vardy amekuwa na kiwango cha juu sana kwa kupachika mabao ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao 15 na kuiwezesha timu yake kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini England.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 ameichezea klabu hiyo mechi 24 msimu huu, pia Vardy alicheza kwenye kikosi cha kocha  Roy Hodgson cha Uingereza kilichofuzu kwa michuano ya Euro 2016.

Aliichezea klabu yake dakika zote 95 katika mechi dhidi ya Bournemouth ambayo walitoka sare ya 0-0 Jumamosi.

Kabla ya kujiunga na Leicester, Vardy aliichezea klabu ya Fleetwood Town.